Karibu Alpha Hostels

Alpha Hostels

Alpha Hostels ni hostel zilizopo mkoani Morogoro, zilizojengwa baada ya kutambua changamoto za malazi zinazozikabili taasisi mbalimbali za Elimu (Shule za Sekondari, pamoja na Vyuo mbalimbali) zilizopo mkoani Morogoro. Taasisi hizo pamoja na kuwa na uwezo mkubwa wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya kufundishia wanafunzi, lakini zimekuwa na uhaba mkubwa wa vyumba vya kulala wanafunzi. Hivyo mnamo mwaka 2013 Hostel hizi zilianzishwa rasmi zikiwa na lengo la kutoa huduma bora za malazi na chakula kwa bei nafuu.

Dira yetu
Huduma bora za hostel zenye kumjali mteja
 
Dhima yetu
Kutoa huduma bora za hostel kwa kuzingatia mahitaji ya Mteja  na Ubunifu.

Shuhuda toka kwa Wateja wetu

Boniphace Sangu Mwanafunzi wa St. August 2016/18

Nilikutana na mazingira tulivu na yakuvutia kwa kusoma, ulinzi & usalama mkubwa, ukarimu, ukaribu kwa wamiliki, kupenda kujua changamoto zilizopo, na kuzikabili kwa wakati. Kila mwanzo na mwisho wa semester na sikukuu zote wenyeji huwa na desturi ya kushiriki pamoja kama familia ya Alpha hostel. Ahsanteni kwa huduma hii na Mungu awabariki.

Maganga Ngassa Former Ma. Ed P. & Admin JUCO Student

Alpha Hostels with well furnished rooms provide an ideal ambience to make residents feel at home. The scenic surrounding, calm and serene atmosphere provide comfortable and conducive environment for learning. Similar I appreciate Alpha Hostels management for facilitating me to finish my studies. Thank you!

Betty Kalungwana Mwanafunzi wa JUCO (2016/17)

Alpha Hostel ni hostel nzuri na ya kisasa, yenye mazingira rafiki kwa mwanafunzi ya kujisomea na huduma zote muhimu zinapatikana kwa bei nafuu kabisaa, sehemu ya kusomea, parking vyumba vizuri vya kulala ambavyo viko full kuanzia vitanda hadi makabati. Kwa bei nafuu inayoendana na uchumi wetu.